13 Juni 2026 - 17:32
Marasimu ya Kumuenzi Ayatollah al-Fayyadh Yafanyika Virginia, Marekani

Kundi la Wanazuoni wa Kiislamu, maimamu wa vituo vya Kiislamu na wajumbe wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia wa eneo la Metropolitan Washington walikusanyika Virginia kumuenzi Ayatollah al-Fayyadh na kuenzi mchango wake wa kielimu na kidini.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Hafla ya kumbukumbu na maombolezo kwa ajili ya Ayatollah al-Fayyadh imefanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Khatam al-Nabiyyin (s.a.w.w.) kilichopo jimboni Virginia nchini Marekani.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na idadi ya wanazuoni wa Kiislamu, maimamu wa vituo mbalimbali vya Kiislamu pamoja na wajumbe wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia wa eneo la Metropolitan Washington.

Washiriki wa hafla hiyo walitoa heshima zao kwa marehemu Ayatollah al-Fayyadh, wakikumbuka mchango wake mkubwa katika nyanja za elimu ya Kiislamu, uongozi wa kidini na huduma kwa Umma wa Kiislamu.

Waliohudhuria pia walisisitiza umuhimu wa kuendeleza urithi wa kielimu na maadili aliouacha Ayatullah al-Fayyadh, huku wakimuombea rehema na daraja za juu mbele ya Mwenyezi Mungu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha